Shahidi wa kwanza katika kesi ya ubakaji inayomkabili mume wa mwimbaji wa muziki wa injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) ameieleza mahakama jinsi alivyobakwa akiwa kwenye gari na nyumbani kwao.
Shahidi
huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni shemeji
wa Mbasha, alidai mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago kuwa Mei 23 mwaka
huu, Mbasha alimbaka kwa mara ya kwanza wakati mkewe Flora akiwa
hayupo.
Alidai
siku hiyo, Flora na mumewe walitoka kwenda kufuatilia CD za video zao
za nyimbo huku mtoto wao (jina tunalo) akiwa shuleni. Alidai alishangaa
kuona ghafla Mbasha alirudi nyumbani peke yake na kumlazimisha kufanya
mapenzi kisha alimtukana na kumtishia kumdhuru endapo atatoa siri.
Akiongozwa
na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, shahidi huyo aliendelea kudai
kwamba Mei 25 mwaka huu, siku ya Jumapili walikwenda kanisani na
waliporudi Mbasha alilalamika kuwa ana njaa hivyo alimpa fedha kununua
chipsi.
Alidai baada ya kula, Mbasha alimwambia waondoke nyumbani kwenda kumtafuta Flora ambaye hakuwepo nyumbani siku hiyo.
“Tulipanda
gari aina ya Toyota Ipsum, wakati tupo njiani aliniambia nikae kiti cha
mbele pamoja naye kwani nilikuwa nimekaa kiti cha nyuma. Nilikubali
kukaa katika kiti hicho ndipo aliniambia kuwa ananipenda hivyo tufanye
mapenzi kwani nimeshazoea,” alidai shahidi.
Aliendelea
kuieleza mahakama kuwa baada ya kukubali kukaa katika kiti cha mbele,
Mbasha alipandisha vioo vya gari na kulaza kiti alichokuwa amekalia
mtoto huyo na kuanza kumvua sketi yake na nguo za ndani. Pamoja na hayo
alimkaba shingo na kumziba mdomo kwa khanga ili asipige kelele na
kumbaka kwa mara nyingine.
Shahidi
huyo alieleza kwamba baada ya kitendo hicho kuisha, Mbasha alishuka
kwenye gari na kumuacha dada huyo akiwa ndani ya gari na aliporudi
alimtaka waendelee kufanya mapenzi kitendo ambacho mtoto huyo alikataa.
Hata
hivyo, alidai baadaye alimtafuta Flora kwa simu na alipopokea
hakumwambia kilichotokea hadi alipofika Sinza kwa dada zake ambako
walimweleza Flora kwa njia ya simu kitendo alichofanyiwa na mumewe, huku
akiwa haamini kilichotokea.
Alidai
walitoka pamoja na dada zake kwenda kuripoti katika kituo cha Polisi
cha Sinza na polisi waliokuwepo kituoni hapo waliwaamuru kutoa taarifa
hizo katika kituo cha polisi ambacho tukio la ubakaji limetokea. Hivyo
walirudi hadi kituo cha Polisi cha Tabata na kutoa taarifa.
Kwa
mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kifungu cha 186,
kifungu kidogo cha tatu cha sheria za mwenendo wa makosa ya jinai sura
ya 20 kinaeleza kuwa mashauri yote ya ubakaji yanatakiwa kusikilizwa
katika mahakama ya siri.
Wakili
Katuga aliiomba mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo katika mahakama ya
siri kwa kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18 na hairuhusiwi mtu
yeyote asiyehusika kusikiliza mashauri hayo. Kesi imeahirishwa hadi
Septemba 12 mwaka huu.
Mbasha
anashitakiwa kwa mashitaka mawili ambayo Mei 23 mwaka huu, maeneo ya
Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala, alimbaka mtoto wa miaka 17 nyumbani
kwake. Pia alidaiwa Mei 25 mwaka huu, alimbaka tena mtoto huyo ndani ya
gari kinyume na sheria.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment