BENKI Kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500 itakayoanza kutumika Oktoba 2014 itakayokuwa mbadala wa Noti ya shilingi 500 inayoonekana kuchakaa haraka.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za
kibenki wa benki hiyo Bw. Emmanuel Boaz wakati wa mkutano na waandishi
wa habari.
“Noti ya shilingi 500 hupita kwenye mikono ya watu wengi zidi na
ndiyo inayotumika zaidi kwenye manunuzi ya kawaida hivyo kuchakaa haraka
ndio maana tumeamua kutoa toleo la sarafu itakayoanza kutumika mapema
mwezi wa 10 mwaka huu.”alisema Boaz.
Akifafanua zaidi Boaz amesema Sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa miaka
mingi zaidi kuliko noti na pia noti zimekuwa zilikaa katika mzunguko kwa
muda mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili
zibadilishwe.
Akitaja sifa za sarafu hiyo mpya Boaz amesema kwanza umbo lake ni la
duara lenye michirizi pembezoni na kipenyo cha milimita 27.5 na uzito wa
gramu 9.5.
Sifa nyingineni kuwa ina rangi ya fedha na imetengenezwa kwa madini
aina ya chuma na Nickel na kwa upande wa mbele ina sura ya Rais wa
kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume na
kwa nyuma ina taswira ya mnyama nyati akiwa mbugani.
Pia Boaz alibainisha kuwa sarafu hiyo kwa upande wa nyuma ina kivuli
kilichojificha ambacho huonesha thamani ya sarafu ya 500 au neno BOT
inapogeuzwa geuzwa.
Kwa upande wa matumizi Boaz amesema sarafu hiyo itakapoanza kutumika
itatumika sambamba na noti za shilingi 500 hadi zitakapokwisha kwenye
mzunguko.
Benki Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la kutoa
sarafu na noti halali (legal tender) zinazotumika nchini ambapo katika
kutimiza jukumu hili Benki kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano
mzuri wa thamani (denomination) unaozingatia uwezekano wa zile zenye
thamani kubwa kuweza kugawika katika zile zenye thamani ndogo
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment