Mwanadada Corazon Kwamboka ambaye kitaaluma ni mwanasheria, raia
wa Kenya anaonekana kutingisha katika soko la umodo Afrika Mashariki
huku baadhi ya warembo wenzake wakimpigia saluti.
Mtandao mmoja wa mambo ya mitindo wa Kenya umeandika kuwa, siku
chache baada ya Corazon kupiga picha zake za mapozi na kuziingiza
mtandaoni, wengi wameonesha kumkubali huku kampuni kibao za mitindo
ndani na nje ya Kenya zikitaka kufanya naye kazi.
Mwanamitindo Corazon Kwamboka.
“Ni mrembo sana, ana umbo namba nane ambalo kila mwanaume atatamani
kumuangalia, amekuwa kwenye midomo ya wengi Afrika Mashariki,” aliandika
katika mtandao huo mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Hassan ‘Hamisa Mabeto’
akionesha kumjua na kumkubali pia.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment