0
Meli ya Australia ikiwa kwenye zoezi la utafutaji wa ndege ya Malaysia iliyopotea kabla ya zoezi hilo kusitishwa.
Mmoja wa ndugu wa abiria waliokuwemo kwenye ndege iliyopotea akilia kwa simanzi baada ya taarifa kuwa ndege hiyo ilianguka kusini mwa bahari ya Hindi.
IDARA ya usalama wa baharini ya Australia imetangaza kwamba shughuli za kuitafuta ndege ya abiria ya Malaysia zimesimamishwa kwa muda kutokana na hali mbaya ya hewa.
Idara hiyo imesema imefanya tathmini na kubainisha kuwa hali mbaya ya hewa itautatiza uchunguzi unaofanywa kutokea angani na majini na inaweza kuyahatarisha maisha  ya marubani.
Uamuzi huo pia unatokana na tangazo la Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak la kuthibitisha kwamba ndege hiyo iliyokuwa inatafutwa imeangukia kusini mwa bahari ya Hindi .
Watu 239 walikuwamo katika ndege hiyo iliyotoweka zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X