Mariah Carey anadaiwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na muongozaji wa filamu, Brett Ratner baada ya ndoa yake na Nick Cannon kuvunjika.
Muimbaji huyo, 44 anadaiwa kuwa karibu na muongozaji huyo, 45, kumsaidia kusahau kuachana na Nick waliyedumu kwa miaka sita.
Carey na Ratner walianza kuwa marafiki baada ya muongozaji huyo kuongoza
video za nyimbo zake Heartbreaker na We Belong Together. Carey pia
aliungana na Ratner kwenye uzinduzi wa filamu ya Hercules aliyoiongoza
na inaaminika kuwa wawili hao walikuwa pamoja kwenye likizo huko Aspen
mwezi December.
Cannon alithibitisha kuachana na Carey mwezi August baada ya miezi
kadhaa ya mgogoro katika ndoa yao na amesisitiza kuwa anachojali sasa ni
wanae mapacha, Moroccan na Monroe.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment