Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuanguka kwa jengo lililopo
kwenye kanisa la TB Joshua jijini Lagos, Nigeria, imefikia watu 115,
kwa mujibu wa serikali ya Afrika Kusini.
Waziri Jeff Radebe wa Afrika Kusini Jumatatu hii ameitaka serikali ya
Nigeria inayokosolewa vikali kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo. Tukio
hilo lililotokea Sept 12 kwenye eneo la kanisa la mhubiri maarufu, T.B.
Joshua, limesababisha vifo vya raia 84 wa Afrika Kusini kutoka kwenye
vikundi vya makanisa yaliyomtembelea.
Ajali hiyo imesababisha uhasama wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kubwa kiuchumi barani Afrika.
Waafrika Kusini wamechukizwa na kile wanachokiona kama serikali ya
Nigeria inajivuta kufanya uchunguzi juu ya kuanguka kwa jengo hilo na
kushindwa kuchukua hatua za haraka kuwaokoa waliokuwa wamenaswa kwenye
vifusi.
Joshua na wafuasi wake wanadai kuwa ajali hiyo ni shambulio
linalohusishwa na ndege ya ajabu iliyokuwa ikipaa juu ya jengo hilo
kabla haijaanguka.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment