Vazi
la Rihanna katika tuzo za mitindo za CFDA mwaka huu limeendelea kuwa
gumzo na wengi wamemshambulia kwa madai ya kutojali maadili.
Member
wa kundi la TLC, Chilli na T-Boz nao hawakusita kumpa makavu live
wakati wanafanya mahojiano na kipindi cha SunRise cha televisheni ya
Australia. Walisema kuhusu mavazi hayo na kueleza kuwa Rihanna anauza
ng9no.
“Ni
vigumu kwetu kusema kitu kwa sababu wakati wowote tukifanya hivyo, ‘oh,
lazima TLC wanaona wivu’, lakini hivyo ndivyo ilivyo. Naliita
koleo..koleo.
“Sisi tuliuza na kuwa kundi kubwa la wasichana la muda wote lililouza zaidi, tukiwa tumevaa nguo zetu. Ni rahisi kuuza ng9no.” Amesema T-Boz.
Ujumbe
umemfikia Rihanna nae hakulaza damu akajibu mashambulizi. Kwanza
alibadili picha yake ya Twitter (Twitter header) na kuweka picha ya
wasichana hao wa TLC, Chilli na T-Boz wakiwa vifua wazi. Katika picha
hiyo wasichana hao wawili wanaonekana wakiwa wamefunika vifua vyao na
mikono.
Baadae
alibadili na kuweka picha yake akiwafanya mzaha na kutoa ulimi nje,
halafu akaiandika, “When there’s no changing the fact that I’m me, and
they’re well…they’re them.”

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment