Macho
na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote
yalielekezwa Durban Afrika Kusini, sehemu ambako zilikua zikitolewa
tuzo za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.
Furaha
tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana wetu toka
nyumbani Tanzania akiwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye tuzo
hizo tena akiwa katika vipengele viwili,ingawa bahati haikuwa njema kwa
Diamond kwani hakufanikiwa kupata tuzo yoyote.
Baada
ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz
ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii:
“Maisha ni Hatua.. Nafikiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema….
“Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next step #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii”.

Diamond
Platnumz alikuwa pia ni mmoja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa tuzo
hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido ilimfurahisha
kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia nyumbani
kupitia DSTV.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment