0

SHEBBY D BLOG

Madereva Bajaj na bodaboda wakiwa nje ya ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar wakipinga tamko la kuzuiwa kuingia katikati ya jiji.Polisi wakiwa eneo la tukio kudumisha ulinzi.
Mmoja wa madereva Bajaj akiongea na vyombo vya habari nje ya ofisi za Chadema.
WAENDESHA bodaboda na Bajaj jijini Dar leo wameandamana mpaka ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zilizopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Nia ya maandamano hayo ni kupinga tamko linalowataka kutopeleka abiria maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar.
Mmoja wa madereva hao, akiongea na wanahabari alisema kwamba wameamua kuandamana mpaka ofisi za Chadema kwa kuwa wanaamini ndio watapata msaada wa tatizo lao.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X