Klabu ya Tottenham imeshakamilisha usajili wa kiungo wa Brazil Paulinho kwa ada ya paundi mil 17 kutoka klabu ya Corinthians. Paulinho ambaye ni kiungo tegemezi wa Brazil alikuwa akiwindwa pia na klabu za Inter milan na Roma lakini mchezaji mwenyewe alichagua kujiunga na Tottenham kwa kile alichokisema ndiyo klabu itakayomuwezesha kukuza kipaji chake zaidi. Paulinho kwasasa yupo na kikosi cha Brazil kwenye michuano ya kombe la mabara na pindi michuano hiyo itakapomalizika ataelekea White Hart Lane kwa ajili ya vipimo na kusaini mkataba na Tottenham. Tottenham ipo juu, kama Bale ataendelea kubaki, basi msimu ujao upinzani wa top four utakuwa mgumu zaidi. |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment