Kikizungumza na Exclusive chanzo makini ambacho
kilishuhudia tukio zima katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni,
jijini Dar kilisema baada ya Amanda kupewa majibu ya vipimo na daktari,
alianza kuhaha huku na kule kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha presha
ikampanda baadaye ikashuka.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu
alimtafuta Amanda na kumuuliza juu ya tukio hilo ambapo bila hiyana
alitiririka:“Ile ilikuwa ni mara ya tatu kupima ngoma yaani wakati nikisubiri majibu, presha ilipanda ghafla mpaka daktari akawa na wakati mgumu wa kunipa majibu.
“Nilienda kuchukua majibu na sikutaka kuyaangalia,
nilimpelekea daktari ambaye aliniambia niko safi yaani sikuamini
nilitoka nikiwa naongea peke yangu, nilikuwa sijiamini si unajua tena
ujana ni maji ya moto sasa presha ,” alisema Amanda.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment