
Diamond Platnumz kipenzi cha mabinti ataungana na star wa Nigeria hit maker wa ‘Dami Duro’ Davido, Ice Prince, Victoria Kimani wa Kenya, na wakali wengine katika ‘Boombaataa Festival’.
Mtandao wa Ghafla umethibitisha ushiriki wa Diamond katika show hiyo kubwa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka nchini Kenya, yenye lengo la kuleta burudani ya utofauti kwa wanamuziki wa Afrika, fashion pamoja na utamaduni.
Show hiyo inategemewa kufanyika (July 27) mwaka huu Nairobi, Kenya.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment