KOCHA mpya wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema atapigana kwa meno na kucha kuhakikisha Cristiano Ronaldo anabakia Real Madrid na kuiepuka Manchester United.
Mwalimu huyo wa zamani wa Chelsea, AC Milan na PSG aliyejiunga na miamba hiyo ya Kihispania hivi karibuni, alisema kwa maoni yake Ronaldo ni mchezaji mkubwa, wa hali ya juu na wa ajabu.
Licha ya Rais wa Real, Florentino Perez kusisitiza kuwa Ronaldo atasaini mkataba mpya, lakini ripoti kutoka Hispania zinadai nyota huyo wa Ureno yuko mbioni kukutana na wakurugenzi wa Manchester United tayari kwa maongezi ya kurejea Old Traford.
Zinedine Zidane (l), Carlo Ancelotti and Florentino Perez
Lakini akizungumza katika utambulisho wake Bernabeu, Ancelotti alisema kwama kwamba Ronaldo ni sehemu ya mipango yake katika safari ya kutaifutia Madrid taji la 10 la ubingwa wa ulaya.
Bosi huyo wa Kiitaliano alisema: "maoni yangu ni rahisi. Ronaldo ni mchezaji wa ajabu.
"Ni heshima kwa kocha kuwa na mchezaji kama Ronaldo kama ilivyokuwa kumkochi Zidane.
"Ronaldo hakuwa katika orodha ya wachezaji kama Ronaldo wa Brazil, Zidane na Ronaldinho ambao niliwahi kuwakochi.
"Yeye atakuwa katika orodha ya wachezaji nitakaowakochi na hilo ni jambo la furaha kwangu."
Ancelotti atakuwa na kauli ya mwisho iwapo kama kuna haja ya Madrid kulipa £ 80m kwa Gareth Bale wa Tottenham.
Na ni yeye pia atakayeamua kumruhusu Gonzalo Higuain kujiunga na Arsenal kwa ada ya £ 20m.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment