Msanii wa muziki wa kizazi kipya Belle 9 amesema hivi sasa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaimba vizuri ila watayarishaji wa muziki wanatakiwa waongeze juhudi katika uandaaji wa kazi za wasanii ili zikidhi hadhi ya kimataifa.

Belle 9 ameiambia Kiss Fm bado hajakiona cha kufanya kwa ambao wapo kwenye game ili muziki wa Tanzania utoke kimataifa kwani mpaka sasa kuna harakati nyingi ambazo zimefanywa na wasanii kama AY,ALLY KIBA na Ben Pol lakini bado haonio kinachoendelea japo wasanii wanaimba vizuri .
“Mimi sijakiona cha kufanya muziki utoke kwasababu mimi namuona AY ndiyo mtu ambae ametoboa lakini muziki ambao anaufanya ni muziki mzuri, lakini nikiangalia kwa watu wengine ambao nikisema tupo kwenye game moja , sioni kitu kipya unajua, so kitu ambacho ninaweza kushauri ili tuwemakini na production zetu ambazo tunazifanya kwasababu kazi zinafika lakini nimeshapata story kazi zinafika lakini zinaonekana demo,” alisema.
“Watu wanakubali video na kunakuwa na ruhusa ya kuchezwa kwenye TV station kubwa kama MTV lakini audio zinatuangusha. Kwahiyo mimi nawasisitiza maproducer ambao wanaanza na wale ambao wapo wajitahidi kufanya kwa quality ambayo itakidhi hadhi ya kimataifa kwasababu kama kuimba tunaimba vizuri.”
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment