1
Habari:
Kila nikiwa na nyoa nywele sehemu za siri baada ya siku kama mbili natokewa na vipele ila kina kuwa kimoja kimoja vinaweza kutoka vipele kama vitatu baadaye kama baada ya wiki kama moja vinaisha je ni tatizo? au? maana vinaninyima raha? 
Na huwa sirudii shavingmachine nikitumia mara moja basi.. Je nitatizo au sababu iko wapi na naomba unishauri nitumie dawa gani...
Jibu  langu:
Tumia  "after Shave" mara baada ya kuondoa nywele hizo. Nyele za kiafrika zimejiviringa/nyonga (curl) hivyo basi unapozinyoa unatakiwa kunyoa na mizizi yake na njia pekee yakufanya hivyo kuhakikisha eneo zima la nywele limelainishwa kwa povu lakutosha la sabuni inayoendana na ngozi yako au "shaving cream" ambayo pia imetengenezwa maalumu kabisa kwa ajili ya aina ya ngozi yako.


Povu la sabuni au "shaving cream" inapopakwa kwenye nywele huingia mpaka kwenye mizizi na kuilainisha na unapopitisha uwembe unakuwa umenyoa nywele zote kutoka mzizini na sio kukata nywele hizo kwa juu-juu tu tendo ambalo husababisha vipele pale nywele zinapoanza kuota tena. Kumbuka kunyoa kila baada ya wiki mbili na usirudie wembe ikiwa unatumia ndio kifaa utumiacho.

Nakaribisha  maoni

Post a Comment

  1. pliz help me natumia magic powder kuondoa ndevu but after kuitumia vipele vinakuwa ving uson

    ReplyDelete

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X