1



Taasisi ya Twaweza imetoa utafiti wake ambao inasema imefanya kwa wananchi wa Tanzania bara kutoka mikoa tofauti ya Tanzania. 
 
Swali la kama uchaguzi ungefanyika leo, ungempigia kura mgombea wa chama gani? wanasema watu wamejibu kama ifuatavyo

CCM - 66%
CHADEMA - 22%
CUF - 1%
ACT wazalendo - 0%
UKAWA - 3%
Kingine - 6%
Hakuna jibu 2%

Utafiti huo  uliotokana na kuhoji watu 1848 kutoka mikoa tofauti ya Tanzania bara, inasema iliwauliza wananchi hao: Ukimwacha Rais Kikwete, iwapo uchaguzi wa urais ungefanyika leo, ungemchagua nani? 

...Majibu ya swali hilo TWAWEZA wanasema limejibiwa na wananchi hao kama ifuatavyo

Magufuli 65 %
Lowassa 25%
Mwingine 3%
Sijui/kataa jibu 7%


Akitangaza utafiti huo leo, Mkurugenzi mtendaji wa TWAWEZA,  Aidan Eiyakuze  amesema kwa upande wa ubunge, Utafiti huo unaonyesha kuwa CCM inaongeza kwa asilimia 60 na kufuatiwa na CHADEMA asilimia 26.

Takwimu zinaonyesha kwamba wananchi hawaelewi nafasi rasmi ya Ukawa




Post a Comment

  1. The lucky club Casino Site
    We've put a lot of hard work into finding luckyclub.live a casino that's the safest place to play and can give you the best possible gaming experience. And with  Rating: 4.9 · ‎46 votes

    ReplyDelete

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X