Rais wa
Nigeria Muhammadu Buhari ametangaza kuwa ana $150,000 (£100,000) kwenye
akaunti zake za benki, katika hatua inayolenga kuendeleza uwazi na
kupiga vita ufisadi serikalini.
Kiasi hicho kinaonyesha kuwa amekuwa
akiishi “maisha ya kujinyima”, msemaji wake Garba Shehu amesema
kuwa, rais Buhari anamiliki makao matano na nyumba mbili za matope,
pamoja na mashamba kadha, akaongeza.
Kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi
alichaguliwa kuwa rais mwezi Machi ahadi zake kuu zikiwa kukabiliana na
ufisadi na ukosefu wa usalama.
Ufisadi ni tatizo sugu katika taifa hilo
lenye uchumi mkubwa barani Afrika na mwezi uliopita, Bw Buhari alisema
$150bn (£100bn) zimeporwa kutoka kwa hazina ya serikali.
Bw Shehu alisema kupitia taarifa kuwa Bw
Buhari ana shamba la matunda na renchi yenye ng’ombe 270, kondoo 25,
farasi watano na ndege wengi.
Pia anamiliki hisa katika kampuni tatu – Berger Paints, Union Bank na Skye Bank, taarifa hiyo iliongeza.
Hata hivyo, makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo ni tajiri kumshinda mdosi wake.
Taarifa hiyo ilisema Bw Osinbajo ana $900,000 (£600,000) kwenye akaunti zake za benki.
Kwenye fomu ya kutangaza utajiri wake,
Bw Osinbajo pia alifichua anamiliki nyumba nne, moja ikiwa ya vyumba
viwili vya kulala ambayo analipia mkopo mjini Bedford, Uingereza.
Taarifa hiyo haikusema thamani halisi ya
mali yote ya rais na makamu wake, ikieleza kuwa stakabadhi
zilizokabidhiwa Afisi ya Maadili zitafanywa wazi kwa umma karibuni baada
ya ukaguzi wake kukamilika.
BBC SWAHILI
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment