Zaidi ya watu 69 wamefariki kwa kunywa pombe yenye sumu Msumbiji, Serikali yatangaza maombolezo siku 3
Afisa afya nchini humo Alex Albertini,
amesema wanaamini kuwa kilevi hicho cha kienyeji kilichotengenezwa kwa
mtama na mahindi kilikuwa na sumu na kuna hatari ya vifo kuongezeka
kutokana na kukosekana kwa vifaa huku watu 196 wakiripoti Hospitali
kupatiwa matibabu.
Uchunguzi wa Polisi umegundua kwamba
pombe hiyo ilikuwa imewekwa sumu ya nyongo ya mamba na kusema wale
waliokunywa wakati wa asubuhi hawakuwa na dalili zozote wakati wale
waliokunywa mchana waliugua na wengine kufariki.
Mwanamke aliyetengeneza pombe hiyo pamoja na ndugu zake nao walifariki.
Sample ya damu za watu waliofariki
imepelekwa Maputo kwa ajili ya vipimo huku Serikali ikitangaza
maombolezo ya siku tatu kutokana na tukio hilo.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment