Raif Badawi ambaye ni mwanzilishi wa Blog hiyo inayoitwa Liberal Saudi Network amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na kuchapwa viboko 1000 hadharani, ambapo kila wiki atakuwa akichapwa viboko 50.
Watu katika mitandao ya kijamii na waharakati wameandika ujumbe wa kuchukizwa kuhusiana na hukumu aliyopewa Blogger huyo kwa kuandika ujumbe wenye hashtags “#FreeRaif, #IStandWithRaif na #JeSuisRaif.“
Mbali na hukumu hiyo, Badawi aliamriwa pia kulipia faini ya dola 226,000 huku mwanasheria wake akihukumiwa miaka 15 jela kwa makosa mbalimbali.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment