Mkusanyiko wa Story kubwa zilizoandikwa kwenye Magazeti ya leo January 13, 2015 nimekuwekea hapa

moreeMWANANCHI 
Harakati za kuwania Urais ndani ya CCM zimeingia katika sura mpya baada ya Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru kuibuka na kudai kuwa wote wanaowania nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa wanatumia fedha kutaka kuingia Ikulu.
Kingunge alisema “kuna suala la kukosa uadilifu, kuna suala la matumizi ya fedha, nikwambie tu ukweli hao wanaotangaza nia wanatumia pesa, wanatumia faulo mbalimbali na wananchi wanajua,”alisema.
Kwa miezi kadhaa sasa makada wa CCM wamekuwa wakitajwa kufanya harakati za chinichini na wengine kushiriki shughuli za wazi zinazoashiria kwamba wanataka kuwania nafasi hiyo ya juu na hadi sasa tayari makada wanne wameweka wazi mipango hiyo.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba kwa nyakati tofauti walitoa kauli zinazowashutumu baadhi ya makada wenzao wa CCM kutokana na matumizi makubwa ya fedha katika ushawishi wa uungwaji mkono.
MWANANCHI
Baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya wamekua wakitumia nyumba za vigogo wakubwa wanazopanga kama kichaka cha kuficha dawa hizo. Imefahamika.
Uchunguzi umebaini baadhi ya dawa za kulevya  wamekua wakipanga nyumba za viongozi ili kukwepa polisi wasiwapekue nyumbani pindi wanaposhukiwa.
Imeelezwa kwamba imekuwa desturi kwa polisi, wakijua kuwa nyumba fulani inamilikiwa na kiongozi fulani wa nchi wanaacha kuipekua kwa kumuheshimu na kudhani kuwa mpangaji ana undugu na kiongozi huyo na wakati mwingine kuogopa tu.
Mkuu wa kitengo cha Polisi cha kuzuia dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alikiri kuwepo kwa suala hilo na kusema kuwa kikosi chake kilifanikiwa baada ya kukiuka utaratibu huo wa kuheshimu  nyumba za viongozi  na kukamata shehena ya unga ikiwa imehifadhiwa katika baadhi ya nyumba.
MWANANCHI
Ikiwa imesalia miezi kumi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa viongozi wa nchi, hadi sasa majimbo sita yako wazi baada ya wabunge wanayoyaongoza kutangaza kutogombea tena ubunge.
Ni wazi kuwa uamuzi wa Wabunge hao, wengi wao wakiwa wameamua kupumzika kwa kushika viti hivyo kwa zaidi ya vipindi viwili, utaibua ‘vita kali‘ vikianza ndani ya vyama wakati wa kura za maoni na baadaye baina ya vyama wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi.
Mbunge aliyetangaza kuachia jimbo hivi karibuni ni Waziri mkuu Mizengo Pinda ambaye ni Mbunge wa Katavi, ambaye alikaa kwa vipindi vitatu tangu 2000.
“Wapo ambao hawatagombea  sababu wanataka kuwania urais,Wapo waliotangaza kutogombea sababu tu ya demokrasia na kutaka kuwapisha wengine,hilo ni jambo zuri“alisema Profesa wa chuo cha Ruaha, Gaudance Mpangala.
HABARILEO
Serikali inakamilisha mpango wa kuzisajili benki za maendeleo vijijini VICOBA ili zitambulike rasmi kisheria.
Kaimu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwekezaji wananachi kiuchumi NEEC, Bengi Issa alisema mpango huo unafanywa kwa sababu Serikali inathamini mchango wa asasi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinasaidia kutekeleza mipango yake ya kuwawezesha wananchi kushiriki katika shughuli za kiuchumi ,zinazolenga kuwakwamua na umaskini.
Aliwaasa Wenyeviti, Makatibu na waweka hazina zaidi ya 140 waliokusanyika kutumia fursa zilizopo nchini za maendeleo na kuwaunganisha wanachama wao pamoja na rasilimali zao ili kuharakisha kuondoa umaskini kwa kununua hisa,kuendesha mfuko wa kuweka na kukopa na kushiriki katika mafunzo ya biashara.
Alisema Vicoba vimekua kimbilio katika masuala ya kiuchumi na kijamii na zaidi ya yote mpango wa vicoba umewezesha wanajamii kujenga tabia mpya na nje ya kujiwekea akiba kidogo kidogo katika kila wiki na baadaye katika benki ya Twiga.
MTANZANIA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein ametangaza rasmi kufuta michango yote katika elimu ya msingi kuanzia Julai mwaka huu.
Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itabeba gharama zote ikiwa kama mkakati wa kuinua elimu.
Alisema hatua hiyo ni mkakati huo ni miongoni mwa njia bora za kuinua kiwango cha elimu Zanzibar, ambapo aliwataka walimu na wazazi kujiandaa kwa kuliendeleza hilo ikiwa ni sehemu ya matunda kwa mwaka 1964.
“Kuanzia mwaka huu elimu ya msingi itatolewa bure,wazee na wazazi pia watatibiwa bure, Serikali ndiyo itakayolipa gharama zote, kuhusu mambo mengine na elimu ya Sekondari vitatolewa maelezo wakati mwingine“alisema Shein.
MTANZANIA
Ndega ya kampuni ya Fastjet imeshindwa kutua Mkoani Mbeya na kulazimika kurejea Jijini Dar es salaam kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa kulikoambatana na ukungu.
Ndege hiyo ilipaswa kutua saa 2 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Songwe na kushindwa kutua na kulazimika kuzunguka hewani zaidi ya mara nbili ikitafuta mwelekeo.
Hali hiyo ilisababisha taharuki miongoni mwa abiria takribani 131 wakiwamo watoto kutokana na ndege kushindwa kutua.
“Tuliogopa baada ya kuona imeanza kuzunguka zunguka hewani na tukaogopa kuwa huenda tukaanguka kwenye safu za milima ya Mbeya“alisema mmoja wa abiria.
Mratibu wa shughuli za ndege wa Shirika hilo Omary Idrisa alikiri hali ya hewa kuchagia ndege hiyo kushindwa kuruka.
MTANZANIA
Mahakama kuu ya kitengo cha biashara imeombwa kutoa amri jengo la Shirika la ndege Tanzania ATCL lipigwe mnada ili kufidia deni la dola za Marekani 1,182,595.38 inazodaiwa na kampuni tatu tofauti.
Kampuni hizo zilizofunguliwa Shirika hilo kesi katika mahakama hiyo, ni kampuni ya huduma za utalii, kampuni ya pembejeo ya Tanzania Bags, na Wellworth Hotel and Lodges.
Wadaiwa hao wanaiomba mahakama iamuru jengo hilo lipigwe mnada baada ya ATCL na Serikali kupitia Wizara ya uchukuzi kushindwa kutekeleza makubaliano ya ulipwaji wa madeni hayo yaliyofanyika baina yake na kampuni hizo Septemba mwaka jana.
Serikali na ATCL ziliahidi kulipa madeni yote kwa awamu tatu,kuanzia Oktoba hadi Desemba 2014, lakini hadi sasa mdaiwa hajalipa.
RAIA TANZANIA
Mtoto mwenye mwaka mmoja, Jafet Mtui mkazi wa Msule, Wilayani Ikungi amekufa kutokana na kunyweshwa pombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Thobias Sedoyeka, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho baada ya mtoto huyo kunyweshwa pombe ya kienyeji baada aina ya Mtukuru akiwa na mama yake Magdalena Muna.
“Pombe hiyo iliandaliwa nyumbani kwa Annastanzia kwa ajili ya shughuli ya kilimo lakini haikunyweka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, hivyo iligawiwa kwa wageni waliofikahapo aiwemo mtoto huyo Jafet “alisema Sedoyeka.
Alisema baada ya mtoto uyo kunywa pombe alitapika na alifariki wakati akipelekwa hospitali na mama yake.
Mama yake pamoja na jirani yao wanashikiliwa na Polisi wakati uchunguzi ukiendelea.

Comments