Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiongea
Kwa Msisistizo Akimtaka Mtendaji wa Kata ya Luhungo Iliyopo Mzee Makame
Kai Kurudisha Fedha za Wananchi wa Kata Hiyo Shilingi Milioni 1.4 Ndani
ya Muda wa Wiki Mbili lasivyo atangulie Polisi.Mh Mbunge Ametoa Kauli
Hiyo katika ziara yake aliyoifanya kata ya Luhungo Kwajili ya Kusikiliza
Kero za wananchi na Ndipo wakazi wa Kata Hiyo walipotoa Malalamiko kwa
Mbunge wao Kuhusu Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata Hiyo Aliyefahamika
kwa Jina la Mzee Makame Kai. Wananchi walimweleza Mbunge kuwa Mtendaji
huyo amechukua fedha za Maendeleo ya Kata Hiyo Kinyume na Utaratibu na
Alipotakiwa kuzirudisha amekuwa na Maneno Mengi Bila Kuzirudisha pia
Kufuja Pembejeo za wakulima Ndipo Mbunge Abood Alipotoa kauli ya
Kumshugulikia kwa Kumpa wiki mbili fedha za Wananchi ziwe zimerudi.
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwasikiliza viongozi wa
Watendaji wa kata ya Luhungo Iliyoo Manispaa ya Morogoro mara baada ya
Kukagua eneo la Ujenzi wa Shule ya Awali Ambapo Mh Mbunge Amechangia
Jumla ya Shilingi Milioni 2
Wakazi
wa Kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro waliojitokeza Kumsikiliza Mbunge
wao Mh Abood aliowatembelea Kusikiliza Kero zao Ambapo wakazi hao
walilamikia Utendaji Mbovu wa Mtendaji wa Kata hiyo Mzee Makame
Kaialiyefuja Fedha za Miradi ya Maendeleo Pamoja na Kuuza pembejeo za
wakulima.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Taarifa za Chama Kutoka kwa Katimu wa CCM Kata ya Luhungo
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza kwa makini Kero
Mbalimbali zinazowasumbua wakazi wa kata ya Luhungo Manispaa ya Morogoro
sambamba akiwa na Diwani wa Kata hiyo kushoto Pamoja na Mwenyekiti wa
CCM Kata ya Lugala Kulia.
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akipokea Taarifa za Maendeleo
kata ya Luhungo Kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa Kata Hiyo
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikagua Kivuko
Kinachounganisaha Mtaa wa Majengo na Mshikamano Eneo la Lukobe Kata Ya
Kihonda Manispaa ya Morogoro wakati wa Mfululizo wa Ziara zake ya
Kutembelea Kata Zinazounda Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Mbunge aliahidi
Kujenga Kivuko Hicho mara baad ya Kutembelea Eneo Hilo na Ndipo wakati
wa Eneo Hilo walipomwomba Mbunge wao Kuwatatulia Kero ya eneo hilo
muhimu inayowaunganisha wakazi wa Mitaa hiyo
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Ujenzi wa Kivuko hicho ambapo
Mpaka ujenzi utakapokamilika Utagarimu jumla ya Shilingi Million 6.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment