Hatimaye Alikiba ameamua kuwajibu baadhi ya wapenzi wa muziki
walioikosoa video ya wimbo wa ‘Mwana’ wanaodai kuwa haiendani na kile
kinachoimbwa.
Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Alikiba amesema
alichokifanya alimaanisha hivyo kuleta picha mpya kwenye vichwa vya
watu.
“Utofauti wa video ndio uzuri wake kwa sababu kila mtu kwenye mind
yake amejenga video, ame-create video itakuwa vipi,” amesema.
Kwa sababu nyimbo imeelezea vitu vingi ni pana kama unavyoona na ina
vitu vingi madawa, ma-prostitute, ukabaji, wizi, vitu fulani vingi sana
nisingeweza vyote kuweka katika video kwa sababu kila mtu anamind yake.
Kwahiyo nilivyofanya utofauti nili-concetrate kwenye dancing na
kucheza na feeling za kuimba. Video nyingi zimeshafanyika duniani sio ya
kwangu tu, kwahiyo watu wasishangae vitendo havikuwepo nimemaanisha sio
nimefanya ili tu nitoe video.”
“Ule utofauti uliokuwepo ndo uzuri wa video yenyewe.
Professionals walifanya hiyo video kwa sababu ni production kubwa iko
na watu ambao wali script vile vile kwahiyo tulishauriana na tuka
appreciate kufanya hicho kitu. Dancing style inaitwa Kalila.
Choreographer wangu ndio alifanya hiyo yote kila kitu.”
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment