USIKU WA WAFALME DAR LIVE: DIAMOND KUTAMBULISHA MADANSA WAPYA


ZIKIWA zimebaki siku tano kamili kuwaka kwa moto wa burudani ndani ya Dar Live, Desemba 25, mwaka huu, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameweka wazi kuwa siku hiyo atawatambulisha rasmi madansa wake wapya.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa katika pozi ndani ya studio za Global TV Online.
Akizungumza katika mahojiano na Global TV Online yaliyofanywa Alhamisi ya wiki hii, Diamond alifunguka kuwa siku hiyo atawaonyesha Watanzania kama anaweza kufanya shoo kubwa ikatambulika kimataifa.
“Niwaambie kuwa mashabiki wangu siku hiyo nitatambulisha madansa wapya. Wategemee kushushudia nikipiga nyimbo zaidi ya 20 bila kupumzika huku nikiwa na wale wote ambao nimeshirikiana nao,” alisema Diamond.
Usiku huo uliopewa Usiku wa Wafalme, atakuwepo pia mkali kunako muziki wa Pwani, Mfalme Mzee Yusuf ambapo siku hiyo ataungana na kundi lake la Jahazi Modern Taarab na kudondosha ngoma kali kibao.

Comments