Nyota wa muziki huo nchini, Rose Athuman Muhando.
LILE jinamizi la kupokea fedha kwa ajili ya kushiriki tamasha la
kuimba nyimbo za Injili kisha kutotokea siku ya tukio linazidi
kumwandama nyota wa muziki huo nchini, Rose Athuman Muhando, safari hii
akidaiwa kumliza tena mtu, Ijumaa Wikienda lina kesi hiyo mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha ndani, safari hii ameendelea kupokea
fedha kutoka kwa mshirika wake kwenye mambo ya Injili, Alex Msama kwa
makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora
mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo
hakutokea!
Chanzo kilisema: “Hivi jamani mnajua kuwa, Rose Mhando amemliza tena
Alex Msama? Amepokea fedha kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Krismasi,
Iringa lakini pamoja na kupokea fedha hizo ameingia mitini.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment