BABA wa nguli
wa filamu Bongo, marehemu Steven Charles Kanumba, Charles Kanumba,
amesema kuwa anaamini kama mwanaye angekuwa hai hadi sasa basi angekuwa
mwanasiasa maarufu nchini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).Akizungumza na Uwazi kwa njia ya simu akiwa kijijini kwao
Shinyanga, Charles alisema, japo imepita miaka kadhaa tangu kutokea kwa
kifo cha mwanaye huyo, bado anawaza ni namna gani angeweza kuleta
maendeleo kwa Watanzania.
“Mwanangu alikuwa na ndoto kubwa ya kuwa mwanasiasa tena kwa kupitia
tiketi ya CHADEMA. Alikuwa akinieleza mambo mengi ya kisiasa lakini kwa
bahati mbaya Mungu alimchukua,” alisema Charles

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment