Yote yalianza baada ya Davido kutweet ‘N they cheat again, Lol’ baada
ya Idris kutangazwa mshindi wa Big Brother Hotshots. Tweet hiyo
ikimfanya Davido atukanwe matusi ya kila aina kutoka kwa Watanzania.
Usiku huo huo, Diamond alishinda tuzo za TFA (The Future Awards) za Nigeria na kuandika:
“Thanks God, we have cheated another one on The Future Awards Africa in Lagos Nigeria… #SameDay #SameNight Thank you Allah.” Ujumbe huo moja kwa moja ukaashiria kuwa jibu kwa Davido ambaye matusi kutoka Tanzania yaliendelea kumsakama.
Baadaye, Davido anayeaminika (na huo ndio ukweli) kuwa msanii
aliyesaidia kumtambulisha Diamond kimataifa, aliandika ujumbe kwenye
Twitter unaoshiria kumlenga Diamond.
“An ungrateful stone will eventually fall… I will always be
grateful to pple that have helped me climb this tall ladder of success,” alitweet Davido.
An
ungrateful stone will eventually fall... I will always be grateful to
pple that have helped me climb this tall ladder of success
— Davido (@iam_Davido) December 8, 2014
Tweet hiyo ilimaanisha: Jiwe lisilo na shukrani hatimaye
huanguka… Nitakuwa mwenye shukrani siku zote kwa watu walionisaidia
kuipanda ngazi ya mafanikio.”
Hata hivyo naye Diamond alitumia siku ya Uhuru wa Tanganyika jana
kutoa nasaha zake kuhusiana na mikwaruzano baina ya wasanii wa Afrika
kwa kuandika:
Badala ya wasanii kuwa ndio mfano bora wa kuweka karibu nchi zao
na kujenga Afrika yenye upendo na amani…eti wao ndio wanakua chanzo cha
kutenganisha nchi zao. Namna hii kweli tutajenga Afrika? Anyway, Happy
Independence day Tanzania.”

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment