Wiki chache baada ya WhatsApp kutambulisha mfumo mpya ambapo iwapo
unamtumia message mtu inakuonyesha alama ya tick mbili za kijani na pia
inaonyesha muda ambao mtu uliyemtumia message hiyo ameisoma, tayari kuna
ndoa ambayo imeingia matatizoni kutokana na hilo.

Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo
kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake
akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message
aliyomtumia yeye hakuijibu.
Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni
dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa
miaka miwili tangu ifungwe.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment