Polisi mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmiliki wa ukumbi wa klabu ya usiku ya Linas Night, Leonard Mtensa (50) ambaye inadaiwa alifariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema Mtensa,
ambaye alikuwa na mpenzi wake kwenye gari maeneo ya Buyekera, alifariki
dunia kabla ya kufikishwa kituo cha afya cha ELCT Ndolage.
Alisema binti waliyekuwa naye kwenye gari anatokea mkoani Mara na kwamba
tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana. Alisema baada ya gari lake
kupekuliwa, vilikutwa vinywaji mbalimbali.
“Baada ya upekuzi ndani ya gari lake, vilikutwa vilevi vya aina
mbalimbali, ikiwamo whisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa, lakini
chanzo cha kifo hicho hakijajulikana,” alisema Mwaibambe.
Kamanda Mwaibambe alisema polisi wanamshikilia mpenzi wake kwa ajili ya
upelelezi kwa hatua zaidi. Kifo hicho kimeshtua wakazi wa Bukoba,
kutokana na mazingira ya kifo cha mfanyabiashara huyo anayemiliki ukumbi
pekee mjini hapa unaotoa burudani hadi asubuhi.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment