Shibuda Anena...."Heri kuwa msaliti kuliko mhaini".....Ampongeza Rais Kikwete kwa usikuvu, Awapiga vijembe CHADEMA
MJUMBE wa Bunge Maalumu, John Shibuda, amesema ni heri kuwa msaliti kuliko kuwa mhaini kwa maslahi mapana ya Watanzania.
Shibuda
ambaye alipewa nafasi kuzungumza baada ya Katiba Inayopendekezwa
kupatikana, alisema anatoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
lakini amepinga kuwa sehemu ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Alisema anajua ataitwa msaliti, jambo alilosema ni vyema kuitwa hivyo kuliko kuwa mhaini wa maslahi ya Watanzania.
Alisema
katika mchakato huo, Rais Jakaya Kikwete amewafundisha Watanzania kuwa
ni msikivu kiasi cha kusikiliza uongo, huku akijua kuwa ni uongo lakini
akaendelea kusikiliza.
Shibuda alisema utumishi wake ni kwa Watanzania na kamwe hauwezi kuwa kwa maslahi ya kikundi cha watu.
Kwa
mujibu wake, Bunge Maalumu la Katiba, limeepuka watu ambao afya zao za
ubongo zina mgogoro, ndio maana wakati wote wanawaza ufedhuli.
Aliwataka
wananchi hao kuwa makini na makatazo ya dini, ambazo zimeasa kuja kwa
zama za manabii wa uongo, ambao alisema siasa imegeuka mfereji wa
manabii hao.
Unataka niwe nakusogezea kila stori inayonifikia zikiwemo pichaz,
video’s na stori zenyewe? niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
twitter na facebook cha kufanya ni kujiunga na mimi kwa
kubonyeza >>> twitter Facebook
Credit Mpekuzi

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment