Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
WAKATI nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’
akikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na
madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila ‘Ray C’
aliyekuwa amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha Polisi cha
Oysterbay, amefuta shauri hilo na kumsamehe.
Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa kauli hiyo muda mfupi
baada ya kuandika waraka katika akaunti yake kwenye mtandao wa
Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi hayo ya madawa ya
kulevya.
Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha kukamatwa kwake na madawa
hayo kitakuwa ni jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama na kumtaka
abadili njia na kuungana naye kwenye tiba ya Methadone kwani ndiyo
kiboko ya madawa ya kulevya.
Kamanda Nzowa.
Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za madawa ya kulevya pamoja na
misokoto miwili ya bangi hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, alikuwa
bado hajafikishwa mahakamani kukabiliana na tuhuma hizo.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment