Picha: Tazama Mashabiki Wa Galatasaray Walivyotia Hasara Emirates Stadium

Klabu ya Arsenal imetoa picha zinazoonyesha uharibifu uliofanywa na mashabiki wa klabu ya Galataray wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa usiku wa kuamkia jana huko jijini London.
Mashabiki wa Galatasaray walionyesha vitendo vya fujo baada ya mambo kwenda tofauti uwanjani kutokana na timu wenyeji kuonyesha uwezo mkubwa dhidi ya kikosi chao na hatimae kufungwa mabao manne kwa moja.
Mbali na uharibibu huo pia mashabiki wa Galatasaray walirusha mafataki uwanjani kwa kuashiria hasira zilizokuwa zinawakabili kutokana na walichokiona katika mchezo huo.

Comments