Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya jana
washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na
kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja
washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna
Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na
Beatus Mmari.
Mdee na
wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote
wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni,
walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka
watawanyike.
Shtaka la
pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa
ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na
sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.






Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment