
Msanii
wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’. Kutokana na wasanii hao
kujitoa, klabu hiyo inaonekana kupoteza muelekeo ambapo kwa sasa
wanachama waliobaki kundini wanajipanga upya ili kuisimamisha upya.
HALI bado tete! Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo
Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kujiuzulu, upepo mbaya
unaendelea kuitafuna klabu hiyo ambapo sasa wasanii wengine watano
wamejiengua, K.Yinakupa mchapo kamili.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wasanii waliojiengua ni Halima Yahya
‘Davina’, Esha Buheti, Kajala Masanja, Flora Mvungi na Salma Salmini
‘Sandra’ hukusababu kubwa ikitajwa kuwa ni kukithiri kwa vitendo vya
ngono na ubaguzi wa kimaslahi.
Kikifafanua madai hayo, chanzo hicho kilikwenda mbele zaidi na kuzinadi kapo hizo kama ifuatavyo:
Cloud 112 (Issa Musa) alidaiwa kuongozana na Coletha Raymond, JB
(Jacob Steven) na Shamsa Ford, Rose Ndauka na Single Mtambalike (Rich)
na wengine.
Davina:
“Mimi nimeamua kujitoa kwa sababu naona mambo mazuri wanachaguana
mapatna tu sisi tunakumbukwa pasipo mazuri, kwenye pesa wanapeana wao
wenyewe, mimi mpaka mume wangu alikuwa akiniuliza kwamba napata faida
gani.”
“Sijapata faida yoyote Bongo Movie, watu wanapeana mapatna inapotokea suala la safari na pesa.”
Esha Buheti:
“Mimi nimeamua kujitoa kwani watu wamekuwa na ubaguzi, sisi tunaitwa
unapotokea msiba tu, nitafanya kazi zangu mdogomdogo, nitatoka tu.”
Msanii wa filamu Bongo, Esha Buheti. Kajala:
“Nimejitoa kwa sababu kule nilikuwa nikimfuata Steve Nyerere, sasa ameshatoka nafuata nini tena?”
Jitihada za kuwapata wasanii wanaotajwa kuwa ni wabaguzi ziligonga
mwamba kwa baadhi ya wasanii lakini alipopatikana Cloud 112, alikanusha
taarifa hizo.
“Hakuna kitu kama hicho, sisi tunasafiri kulingana na matakwa ya
waandaaji wa safari, waandaaji ndiyo wanaosema wanamtaka nani katika
shughuli yao, wanaosema hivyo wamekosa la kuongea,” alisema Cloud 112.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment