Wanawake
MUNGU awasaidie sana Mjue kujenga Mahusiano binafsi ya karibu na MUNGU
mwenyewe kuliko kutegemea sana kuombewa hovyo hovyo,Kisa tu Umeambiwa na
Rafiki yako kwamba yuko Apostle flani ana Upako sana.Ndio ni kweli mna
Matatizo mengi yamewasonga yakiwemo Ndoa zenu Watoto wenu,Biashara
zenu,na Kadharika,Na mara nyingi nia yenu ni kufunguliwa kwenye hivyo
vifungo vinavyowasumbua.Na shetani yuko karibu sana nanyi kwasababu
anajua Nguvu iliyomo ndani yenu, ila wengi wenu hamjielewi.
Ndio maana Mnafanyiwa vitu vingi sana kwa jina la kukombolewa na
baadhi ya Watumishi kwa imani kwamba Mtapona.Na ndio maana kila huduma
maombezi Mmejaa nyie na Ndio maana inakuwa rahisi sana kwenu kudhurumiwa
mambo mengi kwa kujenga imani kubwa sana kwa watu kuliko BABA yenu.
Hebu tazama picha kama hii,Mumeo akikukuta unafanyiwa Maombi ya Staili hii "Atakuelewa kweli!?
Jifunzeni kumlilia MUNGU vyumbani mwenu na Mkumbusheni ahadi zake juu ya Maisha yenu na vizazi vyenu.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment