0




STAA wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefungua kinywa chake na kusema mpenzi wake wa sasa, Nuh Mziwanda ndiye anayemtibu vizuri kunako ‘sita kwa sita’ japokuwa watu wengi wamekuwa wakiudharau mwili wake.
Staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na gazeti hili bila kung’ata maneno, Shilole alisema wengi wanashindwa kujua kwamba mtu anaweza kuwa na mwanaume mwenye umbo kubwa lakini akawa hayajui mapenzi lakini mwenye umbo dogo kama Nuh, akawa ni bingwa wa mapenzi.
Akiendelea kumwaga data mbele ya kinasa sauti cha Amani, msanii huyo anayetamba na wimbo wa Nakomaa na Jiji alisema kuwa katika mapenzi, umri wala ukubwa wa umbo hauna maana yoyote.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
“Yaani kwa kweli Nuh ananimudu na tunaenda sawa katika suala zima la mapenzi, kwa hiyo sioni udogo wake kwangu, kwa upande wangu Nuh ni mkubwa sana watu wasiangalie mwili,” alisema Shilole pasipo kutaja umri wa mpenzi wake huyo.
Shilole aliongeza kuwa, kutokana na mahaba ya nguvu anayoyapata kutoka kwa mpenzi wake huyo, anapata nguvu ya kufanya kazi vizuri siku hadi siku hivyo hapati tamaa.
“Sina stress za mapenzi na mara nyingi nafanya kazi zangu zinaenda sawa kabisa,” alimalizia Shilole.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X