Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amefunguka kuwa kwa sasa hana mpenzi wala hajapata mtu wa kumuoa ila anataka kuolewa na mzee atakayeweza kumlea.
Akizugumza na wanahabari wetu kwenye mgahawa wake wa Ray C uliopo
Mwananyamala, Dar, mwanadada huyo alisema yeye kama mwanamke anatamani
kuolewa na kupata mtoto si na ‘serengeti boy’ bali mzee.
Aliendelea kutiririka kwamba akikosa wa kumuoa atatafuta mwanaume
atakayemlipa kwa ajili ya kuzaa naye tu lakini ni pale atakapokuwa anaweza
kulea mwenyewe.
Ray C aliongeza kuwa, kwa sasa anatafuta wadhamini kwa ajili ya
kuendesha taasisi yake ya Ray C Foundation kwani amefanikiwa kuwasaidia
watu wengi kupata kazi na kuachana na dawa za kulevya.
@Gpl
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment