WANAFUNZI 808,111 wa Darasa la Saba kesho wanaanza mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika kwa siku mbili mfululizo.
Akizungumza
jana Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa
Eustella Bharalusesa alisema idadi hiyo ni kwa wanafunzi wote wanaofanya
mtihani kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Miongoni
mwa hao, 783,223 ni wanaofanya kwa Kiswahili na waliobaki ni kwa
Kiingereza Mwaka jana, wanafunzi wapatao 868,030 walifanya mtihani wa
kuhitimu elimu ya msingi.
Kwa
idadi hiyo ya watahiniwa wa mwaka huu, kunafanya idadi ya watahiniwa
kupungua kwa zaidi ya wanafunzi 59,000. Kwa mujibu wa taratibu za
mitihani ya darasa la saba, jumla ya alama zote ni 250 ambazo hugawanywa
katika madaraja matano yaani A mpaka E.
Mchanganuo uko hivi: Daraja A huanzia alama 201 hadi 250, B inaanzia 151 hadi 200.
Daraja
C ni 101 hadi 150 na D inaanzia 51 hadi 100. Chini ya alama 50 ni
daraja E. Watoto hawa watakuwa zao la pili tangu Serikali izindue Mpango
wa Maendeleo Makubwa Sasa (BRN).
Akizungumzia maandalizi ya mtihani huo, Bharalusesa alisema: “Maandalizi
yamekamilika, usambazaji wa mitihani na vifaa vingine pia
umeshakamilika, hii ni mitihani ina unyeti wake siwezi kusema iko wapi.”
Aidha,
Bhralusesa alisema katika malengo ya BRN, wizara yake ilipanga mwaka
huu kiwango cha ufaulu kiongezeke hadi kufikia asilimia 70.
Katika
mtihani wa mwaka jana, ufaulu ulikuwa ni asilimia 50.51 ikiwa ni
ongezeko la ufaulu kwa asilimia 19.89 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka
2012 ambao ulikuwa ni asilimia 30.72.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment