Beautiful Onyinye, Wema Abraham Sepetu ametoa kioja cha aina yake kwa kuangua kilio baada ya kuambiwa kuwa mbwa wake aliyepotea amepatikana na alipokwenda kumfuata akaambulia patupu.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilitokea juzikati maeneo ya kishua,
Masaki jijini Dar, ambapo staa huyo alionekana kukatishwa tamaa kwani
alipokuwa anatoka nyumbani aliamini kabisa anakwenda kukabidhiwa mbwa
wake aitwaye Vani aliyepotea miezi michache iliyopita.
Nilipoambiwa amepatikana kwanza nilijenga picha kwamba hatimaye furaha yangu imerejea, nilianza
kuvuta picha ya kipindi cha nyuma alipokuwepo nyumbani lakini
nilipokwenda nikakuta ndivyo sivyo,” alisema Wema na kuongeza:
Wema Abraham Sepetu akiwa na mbwa wake, Vanny kabla ya kumpoteza.
“Uwiiii
jamani Vani wangu ndio sitomuona tena naumia sana kuondokewa na Vani
nitamkumbuka daima, sijui amekufa au vipi!” alisikika Wema kiasi cha watu waliokuwepo eneo hilo kumshangaa wakijiuliza ni mbwa tu aliyemsababisha alie kilio mithili ya kuomboleza.
Wema ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa mtu yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake huyo ambaye mwenyewe anasema alikuwa faraja kubwa kwake pindi anapokuwa nyumbani.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment