Kampuni ya Britts Event iliyohusika kuandaa show ya Diamond Stuttgart, Ujerumani imeeleza kwa kina kiini cha vurugu kubwa zilizotokea kwenye show hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa huku baadhi ya watu wakijeruhiwa vibaya.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Awin Williams Akpomiemie
ameeleza kwa kina kuhusu mzozo uliokuwepo ndani ya kampuni hiyo
ulioathiri show hiyo kwa ujumla.
Hiki ndicho alichokisema:
Watu wangu awali ya yote, ningependa kuelezea moyo wangu kwa
kuuambia umma na mashabiki wa Diamond Platnumz, kwamba sisi kutoka
uongozi wa Britts Events tunaomba radhi kwa kile kilichotokea usiku
uliopita, wakati wa show ya Diamond Platnumz.
Haikuwa imepangwa show
ichelewe kuanza au kwa msanii kutotumbuiza. Hapa ntawaeleza ukweli wote
wa kile kilichotokea katika tamasha hilo kwakuwa ninyi nyote mnataka
kuujua ukweli.
Mradi wa Diamond ulikuwa wa gharama kubwa sana kwakuwa uongozi
Britts Events ulitaka kila kitu kiwe professional. Kama kampuni
tuliamua kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye mradi huu hivyo
tuliwafuata wawekezaji watatu lakini mmoja wao hakuwekeza sana kwani
alidai hatokuwa nchini.
Wawekezaji wawili ni watu wanaofahamika sana jijini Stuttgart,
mmoja anafanya kazi na jeshi la Marekani na mwingine anamiliki kampuni
ya usafirishaji mjini Stuttgart. Hawa ndio wawekezaji wakubwa
tuliowapata.
Tuliwapa mikataba wasaini lakini yule mwenye kampuni ya
usafirishaji alikataa kusaini mkataba wa mradi huo kwakuwa alitaka kuwa
na mkataba wake binafsi na yule jamaa wa Marekani. Kisha nilimwambia
Mr.USA kuwa hiyo haikuwa hatua sahihi lakini Mr.USA alisema ‘Britts
msiwe na shaka, kila kitu kitakuwa poa.
Watu wangu, mradi ulianza na kisha wale wawekezaji wawili
wakagundua kuwa Diamond ni msanii mkubwa na angevuta umati mkubwa wa
watu na watu wanampenda.
Kisha walijiunga pamoja dhidi ya Britts
waliowaalika kama wawekezaji kwenye mradi huo na walitaka kuuchukua
kutoka kwa Britts sababu ni wao ndio walioleta sehemu ya fedha kwaajili
ya mradi huu wakati Britts ndio wanaommiliki msanii na mradi wenyewe.
Ila tu kwakuwa Britts ni kampuni mpya mjini Stuttgart, Mr. Shipping Guy
aliamua kuungana na yule jamaa wa Marekani na DJ Wanted, kuuchukua
mradi.
Pindi Britts ilipokaa chini na kufanya mkutano nao, walikuwa
wakifanya mkutano wao wenyewe na kubadilisha mipango yote hivyo walikuwa
wanahujumu na kuendelea na mradi nyuma ya Britts.
Britts ina makubaliano nao kuwa pindi msanii atakapowasili Ujerumani, watampa balance ya 3.250 euros, na walikubaliana na kigezo hicho kwasababu Diamond aliweka wazi kuwa bila fedha asingepanda ndege.
Britts ina makubaliano nao kuwa pindi msanii atakapowasili Ujerumani, watampa balance ya 3.250 euros, na walikubaliana na kigezo hicho kwasababu Diamond aliweka wazi kuwa bila fedha asingepanda ndege.
Waliniomba mimi niongee na Diamond kuwa watampa fedha kwenye
uwanja wa ndege, lakini unajua nini? Kabla Diamond hajawasili Mr. USA na
Mr. Shipping Guy pamoja na DJ Wanted walitaka kuandaa wahuni kumuiba
msanii kutoka kwenye show ya Britts lakini Britts walikuwa wajanja na
walimchukua msanii kabla hawajafanya chochote. Hapo ndipo shida
ilipoanzia.
Huko Essen kabla Britts haijafika huko, USA Guy na Shipping Guy,
walikuwa wameshapeleka wafanyakazi wapya kuchukua show na kuwafukuza
wafanyakazi wa mwanzo.
Kisha Britts ilikuwa ikilumbana nao kuwa wao ni
wawekezaji tu na sio waratibu wa kampuni, kwanini wanataka kuhodhi tukio
kwasababu mnataka kutengeneza fedha na sio kujali watu. Britts baadaye
ilikuja kugundua kuwa wafanyakazi waliowapeleka walikuwa wapenzi wao wa
zamani na ndugu zao.
Dhumuni la kufanya hivyo lilikuwa ni kuiba fedha na kutofuata
mkataba na Britts, hivyo baada ya Diamond kuwasili Stuttgart usiku wa
saa tano, alikuwa amechoka lakini wawekezaji hawakujali. Walikuwa
wakifirikia tu jinsi wanavyoweza kurudisha fedha zao. Diamond alisema
anahitaji fedha yake lakini Shipping Guy na USA Guy walikataa kumpa
fedha Diamond wakihisi kuwa Britts wanataka fedha ya ziada.
Kisha usiku ulipoingia sana, waliweza kutoa 3.000 euros na
ilikuwa saa tisa na nusu tayari lakini Diamond aliendelea kukataa
kutumbuiza kwakuwa alidai ni lazima wamlipe fedha iliyosalia ambayo ni
250 euros, kitu ambacho ni haki yake kutokana na makubaliano.
Mpaka muda Mr Shipping Guy na Mr USA Guy wanagundua kuwa Britts
walikuwa wakifanya kitu sahihi kwa kuwaomba walipe fedha hizo kwa
Diamond, tulikuwa tumeshachelewa na watu walikuwa wameshaanza kupigana
wakati huo Diamond alikuwa ndani ya gari mbele tu ya ukumbi, na kama
ningemruhusu atoke wangemuua.
Tunavyoongea hapa, Mr USA anadai kuwa fedha tulizoingiza kwenye
tukio zima ziliibwa na watu hivyo Britts Events haiwezi kupata fedha
kutoka kwenye tukio tuliloliandaa na kulimiliki. Hiyo ilikuwa mipango
yao kuchukua biashara ya mtu mwingine kutokana na tamaa.
Britts Events inawapenda, Britts Events ilitaka kila mtu awe na
furaha, Britts Event haijawahi kuahidi msanii yeyote na asije. Na
niamini hata tulipofanya show ya Bracket tulikuwa na kitu kile kile
kutoka kwa wawekezaji. Walipoona kuwa show inaweza kuwa na mafanikio
walitaka kupewa asilimia 50% ya kampuni.
Well, sitakiwi kusema yote haya kwakuwa ni jambo la uongozi
lakini niliamua kuweka mambo sawa, siwezi kuficha tena. Tuna Waafrika
wengi wenye tamaa wanaotaka kuchukua biashara za watu wengine sababu ya
tamaa.
Lengo letu ni kuwafanya muwe na furaha na sio kupoteza muda na
fedha zenu. Tunafahamu kuwa nyote mlitoka sehemu za mbali, mliacha
watoto wenu na familia.
Uongozi wa Britts Events unaomba radhi kwa hili. Hivyo msiilamu
Britts Events lakini laumuni tamaa za Mr. USA Guy na Mr. Shipping Guy.
Tunawapenda na tunaahidi show ya bure ya Diamond hivi karibuni.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment