Kwako Kajala Masanja. Bila shaka ni mzima wa afya. Binafsi mimi niko poa na ninaendelea na majukumu yangu kama kawaida.
Leo
nimekukumbuka kupitia safu hii, nataka kuzungumza na wewe, na hasa
katika suala zima la ‘ku-maintain’ ustaa wako.Ninaposema ustaa wako,
namaanisha heshima, kipaji (kazi) pamoja na mapato yako.
Juzi
kupitia gazeti la Ijumaa Wikienda tumeona jinsi gani umepiga hatua
kimaisha. Umetoka katika maisha ya kuonekana wa kawaida, sasa unapewa
heshima ambayo sidhani kama uliwahi kuitegemea kama unaweza kuipata.
Ulikuwa mtu wa karibu na
aliyekuwa shosti wako, Wema Sepetu ‘Madam’ ambaye wakati huo alikuwa ana
mkwanja mrefu kuliko wewe, jinsi fedha ilivyo mwana haramu kwa wakati
huo ilikuwa ikiwezekana kabisa Wema akakutuma kitu, ukatii.
Jeuri ya fedha aliyoionesha
Wema wakati wa matatizo yako alipokutolea shilingi milioni 13, inaonesha
ni jinsi gani mwenzako alikuwa vizuri kifedha. Akakuokoa kwenye kifungo
na wewe ukarudi uraiani.Unakumbuka vizuri hata baada ya yeye kukutolea
fedha hizo nini kiliendelea katika maisha yenu, starehe mwanzo mwisho
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment