Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma leo mchan.
Watu 36 wamepoteza maisha papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya sana.Kwa mujibu wa Ripota wetu aliyekuwa eneo la tukio,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuwa Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni, hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.
Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.
Basi
la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza
linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4
EXPRESS.
Umati
wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya
na kusababisha watu 36 kupoteza maisha wakishuhudia tukio
hilo la ajali.
Guldoza
likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye
nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia
mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na
mmoja kujeruhiwa.
Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.
Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment