Kwa mujibu wa BBC, tukio hilo lilifanyika usiku wa Jumamosi iliyopita na watu takribani 30 walioliokuwa wamewekwa katika kituo hicho kwa lengo la kuangaliwa kama wana dalili za Ebola walitoroka.
Polisi wa Monrovia wameingia mitaani kuwasaka watu hao waliotoroka kwa lengo la kuwarudisha katika kituo hicho huku msako mwingine ukiwa wa kuwasaka waliotekeleza tukio hilo.
Waandishi wa habari walioko nchini humo wamesema inawezakana watu waliotekeleza tukio hilo walichukizwa na kitendo cha serikali kuweka kituo hicho katika mtaa wao.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia pekee, na katika kanda ya Afrika Magharibi ni zaidi ya watu 1,000.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment