0



Rapper T.I anakabiriwa na kesi ya wizi wa vifaa vya jukwaani ambavyo alivikodi mwaka jana wakati wa Tour ya America’s Most Wanted aliyofaya na Lil Wayne na rappers wengine.
Kwa mujibu waTMZ, kampuni iliyomkodishia vifaa hivyo imeeleza katika shitaka lake kuwa ilimkodishia vifaa T.I na akalipia gharama za kukodisha lakini wakati wa kurudisha hakurudisha Screen ya gharama kubwa  inayofahamika kama Roll Drop inayotumika kuonesha picha na video wakati wa show.
Screen hiyo imetajwa kuwa na thamani ya $50,000 lakini kampuni hiyo inataka T.I ailipe $100,000 kwa kuwa katika muda wote iliyopotea ingekuwa imewaingizia kiasi hicho cha pesa kwa kuwakodishia watu wengine.
Tuhuma hizo zinakuja wakati ambapo T.I anaendelea kupiga kazi ya kuandaa albam yake mpya inayoitwa ‘Paperwork: The Motion Picture.
T.I ameeleza katika mahojiano alioyofanya hivi karibuni kuwa albam hiyo itawashikirisha Rick Ross, The Dream, Lil Boosie, Young Jeezy na wengine wengi.
Bado tarehe rasmi ya kutoka haijapangwa.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X