Yamoto Band wapata hisani ya kujiunga na chuo cha Muziki Zanzibar

Wasanii wanaounda bendi ya Yamoto iliyo chini ya Said Fella wamepata hisani ya kujiunga na chuo cha muziki ili kujiimarisha zaidi kiueledi.
Akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, kiongozi wa bendi hiyo, Aslay alieleza kuwa wao wamepata mtu ambaye ameamua kuwapeleka chuo mwezi wa sita mwakani, kitu ambacho wote wamekubaliana nacho.
“Uzuri wote tumemaliza shule form four japokuwa matokeo hayakuwa mazuri. Lakini tuna mpango wa kwenda chuo nafikiri mwakani kama mwezi wa sita tumepanga wote twende chuo ila hatujajua ni chuo gani. Kuna boss fulani siwezi kumtaja jina ametupa ofa tukasomee muziki kule Zanzibar.” Amesema Aslay.
Wiki iliyopita kundi hilo liliachia wimbo mpya walioupa jina la ‘Niseme’

Comments