Serikali imeanza kuingiza nchini vifaa vya kuwabaini watu wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa kali ya ebola ambavyo vitawekwa kwenye viwanja vya ndege pamoja na baadhi ya maeneo ya mipakani.
Jana
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Steven Kebwe alikabidhi
mashine nne za kuwapima abiria wanaoingia nchini kupitia viwanja vya
ndege bila kuwagusa. Vifaa hivyo vinabaini mtu kuwa na dalili za ebola
kutokana na joto lake na abiria wanapimwa kwa kumulikwa machoni na
kwenye masikio.
Kwa
kuanzia mashine hizo ambazo ni mfano wa kamera zitapelekwa kwenye
viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar na Dar es Salaam.
Maeneo hayo kwa mujibu wa naibu waziri huyo ndiyo yanapokea wagonjwa
wengi kutoka nje ya nchi.
Dk
Kebwe pia aliagiza shehena ya mashine zingine zitakazoingizwa nchini
kuanzia leo zipelekwe kwenye viwanja vingine vya Mtwara, Kigoma na
maeneo ya mipakani kuhakikisha kuwa kila abiria anayetoka nje ya nchi
anapimwa dalili za ugonjwa huo hatari.
Pia
aliagiza wanadiplomasia na viongozi wa kitaifa wanaotoka nje ya nchi
ambako wanakwenda kuhudhuria mikutano mbalimbali pia wapimwe kwani
ugonjwa hauchagui cheo wala fedha na hadhi aliyo nayo mtu.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani alisema jana
kuwa wamenunua mashine hizo nne kutoka Afrika Kusini, lakini
zimetengenezwa nchini Marekani kwa kiasi cha Sh milioni 16.
Alisema
katika kipindi hiki ambacho kuna mlipuko wa ugonjwa wa ebola huko
Afrika Magharibi, upatikanaji wa vifaa hivyo ni adimu na haiwezekani
kupata mashine zote kwa msambazaji mmoja, hivyo akasema leo ziwawasili
mashine nyingine mbili kutoka Ubelgiji.
Mkurugenzi
wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga alisema mashine hizo kitaalamu
zinajulikana kama thermo scanners ni mashine za mkononi na kila abiria
atakayeshuka uwanja wa ndege atapimwa kwenye macho au masikio bila
kugusana.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment