KUNDI maarufu la vichekesho ambalo kwa sasa ni kama
halipo, limepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa meneja wao, mtangazaji
nyota wa zamani wa televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven,
kuwamwaga na hivyo kuachana nao.
Baadhi ya waigizaji wa kipindi cha orijino Komedi kutoka kushoto ni Joti, Wakuvanga, Mpoki, Masanja mkandamizaji na Maclegan.
Akizungumza juzikati, Seven alisema ameachana nao
baada ya mkataba wake wa sasa kumzuia kufanya kazi na watu wengine zaidi
ya walio chini ya mwajiri wake mpya.
“Hivi sasa niko na Sony, wao wananizuia kufanya kazi na wasanii ambao hawako nao, hivyo baada ya mkataba wangu na wao kumalizika, nimeamua kuachana nao.
Mimi ni mwakilishi wa Sony barani Afrika, ninashughulika na wasanii toka nchi tofauti za Afrika, kama Senegal, Kenya na kwingineko kasoro Afrika Kusini,” alisema.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment