Muigizaji maarufu na mkongwe katika tasnia ya filamu ‘Hollywood’, mchekeshaji Robin Williams amekutwa nyumbani kwake akiwa amefariki, jana (August 11) majira ya mchana.
Kwa mujibu wa ripoti za polisi wa California, muigizaji huyo aliyekuwa na umri wa miaka 63 alikuwa anasumbuliwa na tatizo la sonona, na msongo wa mawazo na kwamba kwa kuangalia mazingira ya kifo chake anasadikika kuwa alijiua.
Hata hivyo, polisi wameeleza kuwa wamepanga kuufanyia uchunguzi zaidi mwili wake ili kufahamu chanzo cha kifo chake.
“At this time, the Sheriff’s Office Coroner Division suspects the death to be a suicide due to asphyxia, but a comprehensive investigation must be completed before a final determination is made. A forensic examination is currently scheduled for August 12, 2014 with subsequent toxicology testing to be conducted.” Wameeleza polisi wa katika tamko lao rasmi.
Imeelezwa kuwa mara ya mwisho muigizaji huyo alionekana akiwa na mkewe August 10 majira ya saa nne usiku. Huku William akiripotiwa kuonekana kwa mara ya mwisho asubuhi, muda mfupi kabla ya polisi kupigiwa simu.
Robin Williams aliingia rasmi katika tasnina ya uigizaji mwaka 1977 ambapo alitoa filamu ya ucheshi (comedy) inayoitwa ‘Can I Do It ‘Till I Need Glasse’. Kati ya filamu maarufu alizowahi kucheza ni pamoja Mrs. Doubtfire (1991), The Fisher King (1991), Good Will Hunting (1997), One Hour Photo (2002) na filamu ya Hook ya mwaka 1991 aliyoigiza kama Peter Pan au Peter Banning.
Robin ameacha mke na watoto watatu.
Rais wa Marekani Barack Obama ameandika ujumbe kuonesha jinsi alivyoguswa na kifo cha muigizaji huyo ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar ikiwa ni sehemu ya salamu zake za rambirambi.
Huu ndio ujumbe wa rais Barack Obama:
“Robin Williams was an airman, a doctor, a genie, a nanny, a president, a professor, a bangarang Peter Pan and everything in between. But he was one of a kind. He arrived in our lives as an alien - but he ended up touching every element of the human spirit.
He made us laugh. He made us cry. He gave his immeasurable talent freely and generously to those who needed it most - from our troops stationed abroad to the marginalized on our own streets. The Obama family offers our condolences to Robin's family, his friends, and everyone who found their voice and their verse thanks to Robin Williams.”
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment