MAN UTD WAANZA KWA KICHAPO OLD TRAFORD,WATANDIKWA 2 NA SWANSEA


Kocha Mkuu wa Man U, Louis Van Gaal Akishauriana jambo na Kocha Msaidizi Ryan Giggs Kwenye mechi ya Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Swansea
 Mshambuliaji wa Man Utd na Nahodha wa timu ya Man U, Wayne Rooney akigombea Mpira dhidi ya mchezaji wa Swansea city katika Mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza iliyoanza rasmi leo huku Man U ikikubali Kichapo cha Goli 2 Kwa 1 Nyumbani.
 Mchezaji wa Swansea City Sung-Yueng Ki akipongezwa na wachezaji wenzake mara baada ya kuiandikia Timu yake ya Swansea Goli la Kwanza katika Mchezo wa Kwanza wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya timu ya Man U katika Dimba la Old Traford ambapo Man U imekubali Kichapo cha Goli 2 Kwa 1
 
 Nahodha wa Man U Wayne Roone akiwania mpira na Mchezaji Williams Kutoka Swansea katika Mchezo wa Kwanza wa Ligi kuu ya Uingereza uliochezwa leo katika Dimba la Old Traford na Swansea Kuibuka Kinara kwa kuitandika Man U goli 2 kwa 1
 Hatari langoni Mwa timu ya Man U katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza uliochezwa leo huku Man U ikikubali kipigo cha Magoli 2 kwa 1 Nyumbani
 Sung- Yueng Ki mchezaji wa Swansea aliyeiandikia timu yake Goli la Kwanza katika Mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Man U, huku Man U ikikubali kupokea Kichapo cha Magoli 2 kwa 1 Nyumbani.
 Nahodha Wa Man U Wayne Roone Akishangilia goli la Kusawazisha ambalo lilipelekea Timu yake kuwa sare katika Dakika ya 53 ya Kipindi cha Pili. Hadi dakika ya Mwisho Man U ikakubali kipigo cha Goli 2 kwa 1 na Swansea kuibuka Mbabe
 Wayne Roone akiifungia Goli la kufutia Machozi timu yake katika Mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza iliyoanza rasmi leo huku Man U ikipokea kichapo bila kupenda nyumbani dhidi ya Swansea. Picha Kwa Hisani ya BPL na Lukaza

Comments