WAZIRI
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema yupo tayari kufungwa jela kuliko
kuendelea kuwavumilia watu wanaokwamisha ujenzi wa miundombinu ya
barabara kwa kukimbilia mahakamani.
Sambamba
na hilo, pia amepiga marufuku uchimbaji wa mchanga pembezoni mwa mto
uliokuwa eneo la daraja la Lugalo, ikiwa ni pamoja na kuwapa tahadhari
ya kuwafungia wafanyabiashara walio karibu na eneo hilo endapo
watashindwa kuwa walinzi wa uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Hayo
aliyasemwa jijini Dar es Salaam jana, katika ziara yake ya kutembelea
maendeleo ya ujenzi wa miradi ya miundombinu ya barabara pamoja na
madaraja unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Alisema
Serikali imekuwa ikisikitishwa na vitendo vya uharibu wa miundombinu
hiyo vinavyofanywa na baadhi ya watu, licha ya serikali kutumia gharama
kubwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo.
“Watanzania
wanapaswa kujifunza na kuacha ubinafsi katika shughuli za maendeleo ili
kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa katika kiwango kinachostahili, kwa
kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa miundombinu ya barabara.
“Kwa
kiasi kikubwa uharibifu wa miundombinu umechangia kuwepo kwa
ucheleweshaji wa kukamilika kwa baadhi ya miundombinu, kwani hadi sasa
milingoti saba ya taa za barabarani pamoja na mifuniko ya maji taka 12
imeshaibiwa,” alisema Dk. Magufuli.
Kutokana
na hali hiyo, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki,
kuhakikisha anasimamia na kudhibiti vitendo hivyo kwa kuwachukulia
sheria wahusika.
Alisema
Serikali hadi sasa imeshatumia Sh trilioni moja katika kukamilisha
ujenzi wa miradi saba, ambayo ni pamoja na mradi wa barabara za
Mwenge-Tegeta uliogharimu Sh bilioni 89, Morocco Sh bil 288, barabara ya
chini Tazara Sh bilioni 1.2 pamoja na fly over Sh bilioni 100.
Miradi
mingine ni pamoja na ujenzi wa daraja la Kigamboni lililogharimu Sh
bilioni 214, ambapo ujenzi wa madaraja mawili ya Lugalo pamoja na
Mlalakuwa lenye uwezo wa kubeba tani 180, yamekamilika na yameanza
kutumika.
Alisema
pia jumla ya Sh bilioni mbili zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa taa
zitakazotumika katika barabara hizo, ambapo fedha zote zimetokana na
ufadhili wa serikali ya Japan.
Akizungumza
katika ziara hiyo, Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, alisema
serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa
shughuli za kimaendeleo, ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa miundombinu
hiyo.
“Tunatarajia
ujenzi wa mradi wa barabara ya juu (fly over) Tazara kukamilika ifikapo
Oktoba au Novemba pamoja na daraja kutoka Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere hadi mjini,” alisema Okada.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment