Mtoto Rose (kushoto) aliyelawitiwa, na mwenzake Diana aliyetoroshwa na kigogo mmoja aliyetajwa kwa jina la Moses.
****
Wakati watetezi wa haki za binadamu wakizidi kupiga vita matukio ya unyanyasaji wa watoto na wanawake, kigogo mmoja aliyetajwa kwa jina la Moses anadaiwa kumlawiti mtoto, Rose (16) na kumtorosha mwingine aitwaye Diana (12) ambaye ni denti wa darasa la nne.
Kigogo huyo anayesemekana kuwa ni mfanyakazi wa taasisi moja ya
serikali iliyopo jijini Dar (jina tunalihifadhi) alidaiwa kumfanyia
kitendo hicho mtoto huyo ndani ya shamba lake.
Tukio hilo
lilitokea Agosti 20, mwaka huu maeneo ya Zogowale, Kibaha Pwani ambapo
wachunga ng’ombe waliwaona watoto hao wakiwa katika banda peke yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi
karibuni, walisema walitolewa mkoani Lindi kwa ajili ya kufanya kazi za
ndani huku Diana akianika kwamba huyo Moses alimlaghai kuwa angemnunulia
nguo jambo ambalo hakulifanya.
“Mimi nilichukuliwa mwaka jana na kupelekwa Dar kwa ajili ya kufanya
kazi za ndani, baadaye Moses alinitoa na kunihamishia hapa shambani
kwake bila kufanya mawasiliano na wazazi wangu kwani sikuwaaga wakati
nakuja,” alisema Rose.Akaongeza: “Nilishindwa kuwaambia wazazi wangu kwa
sababu alininyang’anya simu halafu akaanza kunilawiti.”
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Jonunga, Mbegu Twaha alisema taarifa
za watoto hao alizipokea kutoka kwa wachunga ng’ombe hao hivyo akaamua
kwenda kwenye shamba hilo na kuwakuta bandani.
Alisema baada ya kufanya mahojiano na watoto hao alibaini kuwa, Rose
alikuwa akilawitiwa na bosi wake, ndipo akaamua kwenda kutoa taarifa
katika Kituo cha Polisi Mlandizi kwa ajili ya fomu ya matibabu (PF3)
ambayo ilionesha kuwa kweli binti huyo alikuwa akiingiliwa.
Kwa ushirikiano na viongozi wengine wa kijiji walifanikisha kuweka
mtego kumnasa mtuhumiwa huyo na kufikishwa polisi ambako alifunguliwa
jalada la kesi lenye Kumbukumbu Na. MLA/IR/1066/2014 KULAWITI.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment